スポンサーサイト

上記の広告は1ヶ月以上更新のないブログに表示されています。
新しい記事を書く事で広告が消せます。

TWENDE ''JINJA'' !!!

JINJA ni aina ya sehemu za kuswali. Huku Japani, JINJA zipo nyingi, unaziona mijini na vijijini, hata milimani na pwani. Sasa, twende JINJA moja tukuonyeshe jinsi tunavyoswali kwa JINJA.

Wakati unapoingia JINJA, unaona TORII, ni geti ya JINJA.

swa-090615-1.jpg

Ukipita TORII, unaona kibanda cha kunawia.

swa-090615-2.jpg

Hapa unawe mikono na mdomo wako ili utulie roho na usafishe mwili wako kabla ya kuswali.
Jinsi unavyonawa ni hivi;

swa-090615-3.jpg1. Chukua kata kwa mkono wako wa kulia na chota maji kwenye beseni, nawa mkono wako wa kushoto.

swa-090615-4.jpg2. Shika kata kwa mkono wako wa kushoto, nawa mkono wako wa kulia.

swa-090615-5.jpg3. Shika kata kwa mkono wako wa kulia, mimina maji juu ya mkono wako wa kushoto, suuza mdomo wako. Usiguse kata moja kwa moja kwa mdomo.

swa-090615-6.jpg4. Nawa tena mkono wako wa kushoto.

swa-090615-7.jpg5. Mwagika maji yanayobaki kwenye mpini, rudisha kata.

Kwa kawaida JINJA inazungukwa na msitu. Ni penye kimya, ukikaa msituni roho inaanza kutulia.
Kutoka TORII, njia inaenda inaelekea jumba la kuswali.

swa-090615-8.jpg

Ukifika mbele ya jumba la kuswali, ugonge kengele, utoe sadaka, uswali.

swa-090615-9.jpg

Jinsi unavyoswali ni hivi;

swa-090615-10.jpg 1. Inama sana mara mbili.

swa-090615-11.jpg 2. Piga makofi mara mbili.

swa-090615-10.jpg 3. Inama tena mara moja.


Haya, umeshajua kuswali kwa JINJA !! Uende ukajaribu siku nyingine.

関連記事

テーマ : アフリカ
ジャンル : 海外情報

コンテンツ一覧

openclose

お問合せはこちらから

名前:
メール:
件名:
本文:

お知らせ
JT☆STARSライブ予定 ・2018.9.29大阪市・The PAX

サイト内検索
リンク
RSSリンクの表示
QRコード
QRコード
上記広告は1ヶ月以上更新のないブログに表示されています。新しい記事を書くことで広告を消せます。