FC2ブログ

Tamasha la NATSU

Mwezi wa saba na wa nane, hali ya hewa ni joto zaidi nchini japani. Ni majira ya joto, tunayoita NATSU.
Watu wakiingia siku za likizo, wanachangamka sana wengine wanakwenda beach, wengine wanatembelea wazee wao, kila mtu anaenjoy natsu yake.

Pia wanakwenda tamasha mbalimbali. Tamasha la Natsu, NATSU-MATSURI inafanyika sehemu nyingi, watu wanajiunga tele! Hasa wapenzi wanapenda kwenda na kushinda pamoja. Wengine wanavaa nguo ya kiasili ya natsu, YUKATA.

Aina za natsu-matsuri ni kama;

HANABI (fashifashi)
Wasanii wa kutengeneza na kuwasha fashifashi wanatuonyesha usanii wao.

swa-090817-1.jpg swa-090817-2.jpg

BON-ODORI
Usiku wanacheza wanazungukazunguka jukwaa, palepale mwinbaji anaimba nyimbo maalum zinazoitwa ONDO, na ngoma zinapigwa. Kila wimbo kuna mtindo wake wa kucheza. Zamani walikuwa wakicheza mpaka asubuhi. Hata leo, wanacheza mpaka asubuhi ingawa inategemea na mahali. hakuna kulala!!

YOMISE
Maduka madogomadogo ya chakula au ya michezo ya kitoto yanayofunguliwa usiku wa natsu-matsuri.

Tunashinda usiku wa natsu hivihivi.

テーマ : アフリカ
ジャンル : 海外情報

Mambo vipi? = Genki?

Habari yako? Leo ninakutamburisha maneno ya salimia!!


Habari za asubii? → O ha yoo
Habari za muchana? → Kon nichi wa
Habari za usiku? → Kon ban wa
Habari yako? → Genki desuka?
Asante → Arigatoo
Kwaheri → Sayoonara

☆☆
Jinalako nani? ⇒ Onamae wa ?
Tutaonana tena ⇒ Matane!!

☆☆☆
Karibu nyumbani! ⇒ Uchi ni asobini kitene!

テーマ : アフリカ
ジャンル : 海外情報

NYAMA CHOMA

TANGAZO

Siku itakayokuja tarehe 9 mwezi wa 8, tutafanya 'NYAMA CHOMA' party OSAKA, JAPAN.
Tunaandaa kupata nyama ya mbuzi au nyama ya kondoo.
Waswahili na wajapani wanaoishi KANSAI wote tunawakaribisha sana.

Sasa tunatafuta pahali pazuri pa kufanyikia NYAMA CHOMA, Tutatangaza hapa baadaye!

Ukitaka kujiunga ututumie message kwa mail fomu chini.

TAARIFA ZAIDI
Tumepata pahali, HATTORI RYOKUCHI, Toyonaka City, Osaka.
Kuna sehemu maalum ya kufanyikia BBQ.
Tunaanza saa 4 asubuhi.

Wageni wote wanakaribishwa.

テーマ : アフリカ
ジャンル : 海外情報

TWENDE ''JINJA'' !!!

JINJA ni aina ya sehemu za kuswali. Huku Japani, JINJA zipo nyingi, unaziona mijini na vijijini, hata milimani na pwani. Sasa, twende JINJA moja tukuonyeshe jinsi tunavyoswali kwa JINJA.

Wakati unapoingia JINJA, unaona TORII, ni geti ya JINJA.

swa-090615-1.jpg

Ukipita TORII, unaona kibanda cha kunawia.

swa-090615-2.jpg

Hapa unawe mikono na mdomo wako ili utulie roho na usafishe mwili wako kabla ya kuswali.
Jinsi unavyonawa ni hivi;

swa-090615-3.jpg1. Chukua kata kwa mkono wako wa kulia na chota maji kwenye beseni, nawa mkono wako wa kushoto.

swa-090615-4.jpg2. Shika kata kwa mkono wako wa kushoto, nawa mkono wako wa kulia.

swa-090615-5.jpg3. Shika kata kwa mkono wako wa kulia, mimina maji juu ya mkono wako wa kushoto, suuza mdomo wako. Usiguse kata moja kwa moja kwa mdomo.

swa-090615-6.jpg4. Nawa tena mkono wako wa kushoto.

swa-090615-7.jpg5. Mwagika maji yanayobaki kwenye mpini, rudisha kata.

Kwa kawaida JINJA inazungukwa na msitu. Ni penye kimya, ukikaa msituni roho inaanza kutulia.
Kutoka TORII, njia inaenda inaelekea jumba la kuswali.

swa-090615-8.jpg

Ukifika mbele ya jumba la kuswali, ugonge kengele, utoe sadaka, uswali.

swa-090615-9.jpg

Jinsi unavyoswali ni hivi;

swa-090615-10.jpg 1. Inama sana mara mbili.

swa-090615-11.jpg 2. Piga makofi mara mbili.

swa-090615-10.jpg 3. Inama tena mara moja.


Haya, umeshajua kuswali kwa JINJA !! Uende ukajaribu siku nyingine.

テーマ : アフリカ
ジャンル : 海外情報

Karibu TABASAMU PLANET!!

Karibu tovuti (website) yetu "TABASAMU PLANET".

Sasa tunaandaa nafasi ya kutambulisha habari za JAPANI kwa kiswahiri.
Tunatakia nafasi hii ikusaidie.

swa-090601-1.jpg

Mlima TEN-NOOZAN, Kyoto

テーマ : アフリカ
ジャンル : 海外情報

コンテンツ一覧

openclose

お問合せはこちらから

名前:
メール:
件名:
本文:

お知らせ
JT☆STARS活動予定
サイト内検索
リンク
RSSリンクの表示
QRコード
QRコード